MSHANA SAMWEL KAWIA CORE

Mshana Samwel Kawia Core-Free PDF

  • Date:08 Apr 2020
  • Views:210
  • Downloads:0
  • Pages:85
  • Size:712.15 KB

Share Pdf : Mshana Samwel Kawia Core

Download and Preview : Mshana Samwel Kawia Core


Report CopyRight/DMCA Form For : Mshana Samwel Kawia Core


Transcription:

UTHIBITISHI WA MSIMAMIZI, Aliyeweka sahihi hapo chini anathibitisha kwamba ameisoma tasnifu hii inayohusu. Kuchunguza Usawiri Chanya wa Mwanamke Katika Vitendawili Vya Jamii ya. Wanyiha na ameridhika kwamba imefikia kiwango kinachotakiwa kuwasilishwa. kwa ajili ya Utahini wa shahada ya Uzamili ya Fasihi kwa Kiswahili Fasihi ya. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Prof Dkt Sheikh T S Y M Sengo. HAKI MILIKI, Tasnifu hii au sehemu yake yoyote hairuhusiwi kukaririwa kuhifadhiwa. Kubadilishwa au kuhaulishwa kwa mbinu yoyote ile kielektroniki kimekanika. kunakilishwa kurudufiwa kupigwa picha au kurekodiwa kwa utaratibu wowote ule. katika hali yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwandishi wake au. kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa niaba yake. TAMKO LA MTAHINIWA, Mimi Mshana Samwel Kawia ninatamka kuthibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi. yangu mwenyewe na kwamba kazi hii haijawahi kuwasilishwa katika Chuo Kikuu. kingine chochote kwa ajili ya shahada hii au tunzo yoyote. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa nami katika. kipindi chote cha masomo yangu mpaka kufikia hatua hii ya kukamilisha utafiti huu. Napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa Msimamizi wangu Prof Dkt Sheikh T. S Y M Sengo wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania kwa kuisimamia kazi hii tangu. mwanzo wa wazo Amenijenga katika taalimu ya kifasihi kwa kunipa mawazo mengi. na kuitalii tasnifu hii katika kila hatua iliyopitia Kwa hakika usimamizi wake. hauwezi kukisiwa wala kulipwa Mwenyezi Mungu Ambariki. Shukrani za dhati ziwaendee wazazi wangu baba yangu Yohna Lulamso Kawia na. mama yangu Prisca Francis Kimario waliojitoa kwa moyo wao wa dhati wa. kunilipia ada katika ngazi za Shule ya Msingi hadi Sekondari bila kujali hali yao. mbaya ya kiuchumi, Naishukuru familia yangu mke wangu Mageni Julius Sagenge na wanangu Brian.
Samwel Kawia na Braiton Samwel Kawia ambao waliweza kuonesha moyo wa. uvumilivu nikiwa katika harakati za kufanya kazi hii Haikuwa rahisi kutimiza. wajibati za kuwa mzazi na kufanya hayo mengine ya kitaalimu bila kuwapunja haki. zao Ahsanteni sana wanangu kwa kunivumilia, Niwashukuru sana wale wote ambao kwa namna moja au nyingine walinisaidia. katika kufanikisha kazi hii baadhi yao walinisaidia katika ukusanyaji wa data za. utafiti huu miongoni mwao ni Raitoni Silwimba Newaho Mera Agrey Nzowa. Siwezi kumsahau Bwana Mgogo Yangson ambaye alinisaidia kufanya tarijama ya. vitendawili vilivyokusanywa kwa lugha ya Kinyiha na kuviingiza katika lugha ya. Utafiti huu ulilenga kuchunguza usawiri chanya wa mwanamke na ujumbe. unaopatika katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha wanaoishi katika wilaya ya. Mbozi mkoa wa Mbeya Tasnifu hii imekusanya vitendawili kutoka katika Kata za. Msia Wasa Igamba na Halungu vijiji vinne vilihusishwa ambavyo ni Igamba. Msia Halambo na Wasa Utafiti huu ulitumia nadharia tatu kwanza nadharia ya. ndani nnje ambayo ilitusaidia namna ya kuingia masikanini na kumakinika na. wenyeji kiasi cha kupunguza ugeni wa mtafiti Nadharia hii ilimsaidia mtafiti. kupata uhusiano mzuri kati yake na watafitiwa Pili Nadharia ya ufeministi. ilituongoza kuchunguza namna jamii ya Wanyiha inavyowasawiri wanawake katika. mfumo mzima wa maisha Tatu Nadharia ya uhalisiya ilituongoza kuchunguza. ujumbe unaopatikana katika vitendawili vya jamii ya Wanyiha Nadharia ya. ufeministi na uhalisia zilikuwa mwafaka katika hatua ya uwasilishaji na uchambuzi. wa data Mbinu tatu zilitumika katika hatua ya ukusanyaji wa data Mbinu ya. mahojiano mbinu ya umakinifu na mbinu ya Udurusi wa nyaraka maktabani Jumla. ya vitendawaili arobaini vilikusanywa vitendawili vitano viliteuriwa ili kutusaidia. kutafuta majibu ya utafiti huu Utafiti umepata majibu kwamba vitendawili katika. jamii hiyo humsawiri mwanamke katika hali mchanganyiko chanya na hasi Kwa. hiyo utafiti wetu umepata majibu kwamba vipo vitendawili vyenye mtazamo. chanya kuhusu mwanamke Ujumbe unaopatikana katika vitendawili ni kwamba. mwanamke anapaswa kuthaminiwa sawa na mwanaume,UTHIBITISHI WA MSIMAMIZI ii. HAKI MILIKI iii,TAMKO LA MTAHINIWA iv,SHUKRANI v,IKISIRI vi. JEDWALI xi,KIELELEZO xii,SURAYA KWANZA 1,UTANGULIZI 1. 1 1 Utangulizi wa Jumla 1,1 2 Utangulizi wa Utafiti 3.
1 3 Usuli wa Tatizo la Utafiti 4,1 4 Sababu za Uteuzi wa Mada 6. 1 5 Tatizo la Utafiti 7,1 5 1 Lengo la Utafiti 7,1 5 2 Madhumuni Maalumu ya Utafiti 7. 1 5 3 Maswali ya Utafiti 7,1 6 Umuhimu wa Utafiti 8. 1 7 Eneo la Utafiti 8,1 7 1 Mipaka ya Utafiti Kijiografia 8. 1 7 2 Eneo la Kitaalimu 8,SURA YA PILI 9, UTALII WA KAZI TANGULIZI NA MKABALA WA KINADHARIA 9.
2 1 Utangulizi 9, 2 2 Ufafanuzi wa Dhanna kama Zilivyotumika Katika Kazi Hii 9. 2 2 1 Jinsia 9,2 2 2 Vitendawili Ivhili 10,2 2 3 Usawiri 12. 2 2 4 Mapitio kuhusu Usawiri wa Mwanamke Katika Fasihi 12. 2 2 4 1 Ujumbe wa Vitendawili Katika Jamii 18,2 3 Nadharia za Uhakiki 20. 2 3 1 Nadharia ya Ndani Nnje 21,2 3 2 Nadharia ya Ufeministi 22. 2 3 4 Nadharia ya Uhalisiya 25,SURA YA TATU 28,MBINU ZA UTAFITI 28.
3 1 Utangulizi 28, 3 2 Njia Zilizotumika Katika Ukusanyaji wa Data 28. 3 2 1 Njia ya Mahojiano 29,3 2 2 Njia ya Umakinifu 29. 3 3 Wasaidizi wa Ukusanyaji wa Data 30,3 4 Zana za Utafiti 31. 3 4 1 Kalamu na Karatasi 31,3 4 2 Kirimbo 31,3 4 3 Simu ya Mkononi Rukono 31. 3 4 4 Ngamizi 32,3 5 Vyanzo vya Data 32,3 5 1 Data za Msingi 32.
3 5 2 Data za Upili 32,3 6 Uteuzi wa Walengwa 33,3 6 1 Njia za Kupatia Walengwa 33. 3 6 2 Njia ya Uchambuzi wa Data 34,3 7 Hitimishi 36. SURA YA NNE 37,UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA ZA UTAFITI 37. 4 1 Utangulizi 37,4 2 Uwasilishaji wa Data 37, 4 3 Usawiri Chanya wa Mwanamke Katika Vitendawili vya Jamii ya Wanyiha 38. 4 3 1 Mwanamke Anasawiriwa Kama Mama Mlezi wa Watoto Katika Jamii 38. 4 3 2 Mwanamke Kiumbe Mvumilivu 40, 4 3 3 Mwanamke Anastahiki Kupewa Hadhi Katika Jamii 42.
4 3 4 Mwanamke ni Kiumbe Mchapakazi Katika Jamii 44. 4 3 5 Ujumbe Unaopatikana Katika Vitendawili vya Wanyiha 48. 4 3 5 1 Mama ni Mlezi wa Watoto 49,4 3 5 2 Mwanamke ni Mvumilivu Katika Jamii 51. 4 3 5 3 Mwanamke ni Mvumilivu kwa Mume Wake 52,4 3 5 4 Uvumilivu Kipindi Cha Malezi ya Mtoto 52. 4 3 5 5 Mwanamke ni Mzazi Anayestahiki Kupewa Hadhi 54. 4 3 5 6 Mwanamke ni Mchapakazi Katika Jamii 56,4 4 Hitimishi 57. SURA YA TANO 59,MUHTASARI MATOKEO YA UTAFITI NA MAPENDEKEZO 59. 5 1 Utangulizi 59,5 2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti Huu 59.
5 2 1 Usawiri Chanya wa Mwanamke 59, 5 2 2 Ujumbe Katika Vitendawili vya Jamii ya Wanyiha 60. 5 3 Mambo Mapya Katika Utafiti Huu 60,5 4 Mapendekezo 61. 5 4 1 Mapendekezo kwa Wanazuoni 61,5 4 2 Mapendekezo kwa wanajamii 61. 5 4 3 Mapendekezo Serikalini 61,MAREJELEO 62,VIAMBATANISHI 67. Jedwali Na 3 1 Uteuzi wa Wahojiwa 34, Kielelezo Na 1 1 Ofisi ya Mapokezi Kwenye Eneo la Kimondo 2.
SURAYA KWANZA,UTANGULIZI,1 1 Utangulizi wa Jumla, Mbozi ni miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Mbeya Ipo Kusini Magharibi mwa. Mkoa wa Mbeya kati ya latitudo 8o hadi 12o Kusini mwa Ikweta longitudo 12 3o na. 33 2o Mashariki mwa Greenwich Upande wa Kusini inapakana na Wilaya ya Ileje. Mashariki hupakana na Wilaya ya Mbeya Vijijini katika ukingo wa Mto Songwe. Upande wa Kaskazini hupakana na Wilaya ya Chunya upande wa Magharibi. hupakana na Wilaya ya Momba na nchi ya Zambia, Wenyeji wa wilaya hiyo ni Wanyiha lakini kuna jamii za wahamiaji k v Wandali. kutoka wilaya ya Ileje Wanyakyusa kutoka wilaya ya Rungwe na Wanyamwanga. kutoka wilaya ya Momba Wanyiha wanaishi nyanda za juu kati ya mita 900 2700. juu ya usawa wa bahari hasa katika Tarafa tatu za Vwawa Igamba na Iyula Ardhi ya. Unyihani ni nyekundu lakini yenye rutuba inayostawisha mazao yakiwamo ya. chakula k v mahindi maharage ndizi karanga na biashara hasa kahawa Ndani ya. eneo hilo kuna kimondo chenye umaarufu mkubwa duniani kikiwa na uzito wa tani. kumi na mbili Kipo katika Kijiji cha Ndolezi ni kivutio ambacho mpaka sasa. Serikali haijafanya jitihada zozote za kuwekeza kwani hata ofisi ya kufikia na. kupumzikia wageni wafikao hailingani na hadhi ya kimondo chenyewe. Kimondo ambacho kilidondoka kutoka angani huko Mbozi Mbeya karibu na mji wa. vwawa Kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na kilianguka katika mlima wa. mlenje Kimondo hicho ni kimoja kati ya vimondo 10 vinavyojulikana duniani na. kina urefu wa mita 3 3 na urefu wa mita 1 63 na kimo cha 1 22. Kielelezo Na 1 1 Ofisi ya Mapokezi Kwenye Eneo la Kimondo. Chanzo English Version 2012, Kwa upande wa umbile kimondo hichi kiko tofauti na vimondo vingine. vinavyopatikana ulimwenguni kwa sababu kimondo hichi ni hasa kwa chuma. Chuma kimechukua asilimia 90 45 na nikel asilimia 8 69 sulfuri asilimia 0 01 na. fosfori asilimia 0 11 ya masi yake Kuna umuhimu kwa wizara husika kuitangaza. sehemu hiyo kibiashara ili kupata watalii ndani na nnje ya Tanzania Watalii kutoka. Duniani kote wanaokuja kuangalia mbuga za kusini mwa Tanzania wataweza. kwenda kuangalia hazina yetu kubwa ya tani 16 iliyoanguka katika eneo la Mbozi. miaka zaidi ya 1 000 iliyopita na kuchimbuliwa miaka ya 1930. Jamii ya Wanyiha ni miongoni mwa jamii za kale hapa nchini ambayo ina historia. ya muda mrefu tangu kipindi cha maisha ya utangu hadi sasa kwa msingi huo jamii. ina mambo mengi mema ambayo ni vema yakakusanywa na kuhifadhiwa kwa. manufaa ya wanajamii katika vizazi vingi vijavyo Miongoni mwa mambo hayo ni. pamoja na tanzu za fasihi simulizi zilizosheheni vijitanzu kadha wa kadha vikiwemo. vitendawili,1 2 Utangulizi wa Utafiti, Utafiti huu ulikusudiwa kuchunguza usawiri chanya wa mwanamke katika. vitendawili vya jamii ya Wanyiha waishio wilaya ya Mbozi Ili kufikia lengo. lililokusudiwa vitendawili viliainishwa na kuchambuliwa kisha kumeoneshwa. mhusika mwanamke anavyosawiriwa kwa mtazamo chanya katika kazi hizo. Wanazuoni waliovutiwa kuchunguza usawiri wa mwanamke katika fasihi simulizi. vikiwamo vitendawili wameonesha kwamba mwanamke anapewa mtazamo hasi na. jamii Hali hiyo imekuwa ni chanzo cha wanawamke kuendelea kuishi maisha ya. utegemezi wa kiakili na kiuchumi kutoka kwa wanaume Usawiri chanya wa. mwanamke katika vitendawili haujazungumzwa kwa kina cha uzamili au uzamivu. Utafiti huu umelenga kushughulikia kipengele hicho kwa upana wake. Utafiti huu ulitumia nadharia tatu kwanza nadharia ya ndani nnje ambayo. ilitusaidia namna ya kuingia masikanini na kumakinika na wenyeji kiasi cha. kupunguaza ugani wa mtafiti Nadharia ya ufeministi ilituongoza kuchunguza namna. jamii ya Wanyiha inavyowasawiri wanawake katika mfumo mzima wa maisha. Tatu Nadharia ya uhalisiya ilituongoza kuchunguza ujumbe unaopatikana katika. vitendawili vya jamii ya Wanyiha, Njia tatu zilitumika katika ukusanyaji wa data kwanza njia ya mahojiano ilitusaidia.
kupata ufafanuzi wa kina kutoka kwa watafitiwa Pili njia ya umakinifu ilitusaidia. Vitendawili vilianza kutumika zamani sana tangu binadamu alipoanza kutumia lugha kama chombo kikuu cha mawasiliano Vitendawili vililenga kupanua ujuzi wa hadhira katika elimu ya mazingira yake pamoja na kukuza wepesi wa kuwaza na kuchemsha ubongo Vitendawili ni amali ya jamii ambayo hurithishwa kutoka kizazi

Related Books