KUHANI MKUU cdn ministerialassociation org

Kuhani Mkuu Cdn Ministerialassociation Org-Free PDF

  • Date:29 Feb 2020
  • Views:204
  • Downloads:0
  • Pages:68
  • Size:546.75 KB

Share Pdf : Kuhani Mkuu Cdn Ministerialassociation Org

Download and Preview : Kuhani Mkuu Cdn Ministerialassociation Org


Report CopyRight/DMCA Form For : Kuhani Mkuu Cdn Ministerialassociation Org


Transcription:

ukurasa ili kila mmoja wa kikundi awe na ukurasa mmoja ili kufuatiza wakati wa. Makanisa ulimwenguni yataunganika katika maombi haya kila siku katika mada ya. siku Jiunge katika maombi kupitia kwenye Maandiko nukuu na mahitaji ya maombi. yalioorodheshwa kila siku Hata hivo usije ukalazimika kupitia orodha yote ya mahitaji. yaliyoorodheshwa ili kuombewa Mnaweza kugawanyika katika vikundi husika na kila. kikundi kuombea baadhi ya mambo katika ile orodha, Baadhi ya mahitaji katika orodha ya maombi yanamhusu mtu mmoja mmoja na. mengine yanalihusu kanisa la Waadventista wa Sabato la ulimwengu Ni muhimu. kuomba pamoja kwa ajili ya mahitaji ya pamoja kama familia ya kanisa lakini. mnaweza kuchagua muda wa kuomba mnaoona unafaa na kuombea mambo ya. kawaida hasa ikiwa kuna wageni ambao sio Waadventista wa Sabato Ombea namna. mnavyoweza kupata njia nzuri za kualika wageni na kuwafanya wajisikie sehemu ya. kikundi chenu, Nukuu za Ellen G White kuhusu ishara zilizoko katika vazi la Kuhani Mkuu Hapa. pameorodheshwa nukuu kutoka katika maandiko ya Ellen G White na baadhi ya. mafungu kila moja ya siku hizi kumi Nukuu hizi pamoja na mafungu ya Biblia. zinaelezea kile kinachowakilishwa na mavazi mbali mbali ambayo Kuhani mkuu. alikuwa akivaa Inapendekezwa kwamba msome nukuu na mafungu haya pamoja. katika kikundi chenu Mnaweza kufanya hivi kabla ya maombi ili kujenga hoja kwa ajili. ya mada husika au kati kati ya kipindi cha maombi, Muda unaopendekezwa kwa ajili kila kipengele cha maombi Muda utakaotumia kwa. maombi unaweza kutofautiana kila wakati mnapoomba pamoja Yafuatayo ni. mapendekezo yanayoweza kuwa bora,Kukaribisha Utangulizi dakika 2 hadi 5. Kusoma mafungu na nukuu za maandiko ya EGW dakika3. Kipindi cha ibada ya kusifu katika maombi dakika 10. Kipindi cha toba na kuungama pamoja na kudai ushindi dhidi ya dhambi. dakika 3 hadi 5, Kipindi cha kujitoa na kuingilia kati kwa maombi dakika 30 hadi 35.
Kipindi cha shukrani katika maombi dakika 10, Kumsihi Mungu na kuomba kwa ajili ya watu saba uliowachagua Watie moyo watu. wote kumsihi Mungu awaoneshe kila mmoja watu saba ambao atakuwa anawombea. katika siku hizo kumi za maombi Wanaweza kuwa ni wanafamilia marafiki. wafanyakazi wenza washiriki wenzako kanisani n k Wahimize waombe kwamba. Roho Mtakatifu awaongoze hao watu saba wadumu katika Kriso Wanakikundi pia. wamwombe Mungu awaoneshe jinsi watakavyoombea mahitaji mahususi ili kuwafikia. hao watu saba kwa kipindi hiki cha siku kumi za maombi. Huduma ya Sabato katika siku hizi kumi za mwaka 2018 Maombi na yalenge katika. kitu mahsusi mkishiriki shuhuda mbali mbali jinsi Mungu alivyojibu maombi Jambo. hili linaweza kufanyika katika vipindi mbali mbali katika Sabato mbili hizo Ni vema. kuwa wabunifu kuhusisha familia nzima ya kanisa kile ambacho kimekuwa. kikitendeka katika mikutano ya maombi siku hizo kumi. Sherehe za Sabato ya kuhitimisha Sabato ya mwisho ipangwe mapema uwe ni wakati. wa kujumuika katika furaha ya mambo yote aliyoyatenda Mungu katika kipindi hiki. cha maombi ya siku kumi Tenga muda wa kutosha kwa ajili ya ushuhuda wa maombi. yaliyojibiwa kwa ajili ya mafundisho maalum ya Biblia mahubiri yaliyotayarishwa. vizuri kuhusu umuhimu wa maombi na nyimbo za sifa kwa Mungu wetu Kusanyiko. liongozwe katika wakati wa maombi ili wale ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria. katika siku hizi washiriki uzoefu wa furaha ya kuomba na wengine Somo la siku ya. kumi na moja lina dhana husika, Kufuatilia kipindi hiki cha maombi ya siku kumi mwaka 2018 Omba sana ili kujua. jinsi Mungu anavyotaka kanisa lako au kikundi chako kiendeleze kile ambacho. Amekianzisha katika siku hizi kumi za maombi Pengine ni vema kuendelea na. mikutano ya maombi ya kila wiki au labda Mungu anataka uanze huduma mpya. katika kanisa lako au utoke kuwaendea wengine katika jamii Uwe muwazi na kufuata. kile ambacho Mungu anaelekeza Utashangaa kadiri unavyotembea naye. Ushuhuda Ni vema kushiriki visa vyako jinsi Mungu alivyotenda kupitia kwako katika. siku hizi kumi za maombi ya mwaka 2018 Visa vyako vitawatia moyo wengine Visa. hivi vinaweza kutumwa katika Idara ya huduma binafsi kwa baruapepe iitwayo. stories ministerialassociation org au kutumwa moja kwa moja kwenye tovuti ya. www tendaysofprayer org,Vielekezi vya kuunganika katika maombi. Kubalianeni, Wakati mtu mmoja anapokuwa akimwomba Mungu kwa ajili ya hitaji fulani hawa. wengine nao waendelee kuomba kimya kimya na hivyo maombi yanaunganika. pamoja Sio kweli kwamba mtu mmoja akiombea haja fulani basi wengine hawa. wanabaki wamenyamaza tu bali wnatakiwa kuunganika katika maombi huko ndiko. kupatana katika maombi Tunasoma katika Mathayo 18 19 kuwa Tena nawaambia ya. kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba. watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni Unapotegemezwa wakati wa maombi. katika hitaji fulani basi inatia moyo,Kudai Ahadi za Mungu.
Kuna ahadi kadhaa za Mungu zimetayarishwa ili kusaidia watu kudai katika maombi. Wahimize wanakikundi kudai ahadi za Mungu kadiri wanavyoomba Ni rahisi. kujielekeza katika matatizo yetu lakini tunapodai ahadi za Mungu basi tunaongeza. imani yetu na kujikumbusha kwamba hakuna jambo gumu lisilowezekana kwa Mungu. Ahadi zinatusaidia kuondoa fikra zetu katika madhaifu na magumu yanayotukabili na. kuzielekeza kwa Yesu Kuna ahadi katika Biblia ya kudai tunapokabiliana na. changamoto fulani Wahimize washiriki katika vikundi kutafuta ahadi zaidi na. kuziandika ili kuweza kuzidai siku za usoni, Tunatakiwa kuwasilisha mahitaji yetu kwenye maombi kwa moyo wa unyenyekevu. na kuzieleza kwa uwazi na uhakika huku tukidai ahadi kwa imani hadi kusanyiko. zima watambue kwamba tumejifunza kudumu kumsihi Mungu katika maombi. Watatiwa moyo kuanimi kwamba kuna uwepo wa Bwana katika mkutano kisha. watafungua mioyo yao ili kupokea mibaraka yenye utajiri Imani yao itaongezeka nao. watakuwa tayari kusikiliza maagizo yanayotolewa na mzungumzaji kwa masikio. yenye utayari Evangelism uk 146, Mungu ametayarisha mbingu iliyojaa mibaraka kwa wale ambao watashirikiana naye. Wale wote wanaomtii wanaweza kudai kwa ujasiri kutimizwa kwa ahadi zake Lakini. ni lazima tuoneshe uimara usio yumba yumba wa imani kwa Mungu Mara nyingi. anachelewa kujibu maombi yetu ili kujaribu imani zetu na udhati wa matumaini yetu. Baada ya kuomba sawasawa na Neno lake tunatakiwa kuamini katika ahadi yake na. kudumu kusihi kwa dhati naye hatatukatalia Christ s Object Lesson uk 145. Wakaribishe wale mliojiunga katika maombi ya siku kumi za maombi katika aina moja. au nyingine ya kufunga kwa mfano kuepuka kuangalia TV kwa kipindi fulani muziki. intaneti mitandao ya kijamii vitafunwa vitamu vitamu au vyakula aina ile inayokuwa. ngumu kumeng enywa Tumia wakati wa ziada kujifunza Biblia zungumza na Mungu. na kumwomba awasaidie katika kikundi chenu na kusanyiko lote kwa ujumla ili. kudumu kwa utimilifu ndani ya Kristo Kwa kutumia lishe ya kawaida iliyo rahisi. hawa wanakikundi wataruhusu fikra zao kupata uweo wa kusikia na kupokea sauti ya. Roho mtakatifu,Roho Mtakatifu, Ni vema kuwa na uhakika kwamba tumemwomba Roho Mtakatifu atuoneshe jinsi ya. kuomba na mambo ya kuombea katika maisha kwa hali fulani mahususi Biblia. inatuambia kwamba hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini Roho mwenyewe. hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, Hatuna budi kuomba sio tu kwa jina la Yesu Kriso bali pia kwa uvuvio wa Roho. Mtakatifu Kufanya hivi kunaelezea maana ya kusema Roho Mtakatifu hutuombea kwa. kuugua kusikoweza kutamkwa Warumi 8 26 Mungu anafurahia kujibu maombi. kama hayo Tunapopumua maombi kwa udhati wa pekee kwa jina la Kristo panakuwa. na ahadi kutoka kwa Mungu kwamba anaenda kujibu hayo maombi kama. ilivyoandikwa Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote. tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu Waefeso 3 20. Christ s Object Lessons uk 147,Kuwa Pamoja Kimwili.
Mnapoanza kuingia katika maombi ya kuunganika karibisha kila mmoja aje kushiriki. Watu wanapounganika pamoja katika mduara ulio imara inasaidia kukuza roho ya. umoja ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya maombi ya muunganiko Ikiwa watu. watatawanyika katika chumba itakuwa ni vigumu kusikilizana wakati wa maombi. Kutunza taarifa ya maombi, Zoezi la kutunza taarifa ya maombi katika siku hizi kumi litakuwa ni namna iliyo nzuri. ya kushiriki kuzamisha zile mada za kila siku katika fikra za wanakikundi na kusaidia. katika kufanya maamuzi thabiti kwa Mungu na kutambua mibaraka yake kwao. Kuorodhesha maombi yaliyofanywa na kutunza taarifa ya maombi yaliyojibiwa ni. namna iliyothibitishwa ya kutia moyo, Kuna namna kadhaa mabazo unaweza kujumuisha hii orodha katika maombi haya ya. siku kumi Unaweza kutenga muda wakati wa maombi ili wanakikundi waorodheshe. maombi yao na jinsi Mungu alivyowajibu Au unaweza kutunza yale mambo. mnayoombea na ikiwa yamejibiwa basi kuyaweka kwenye bango kubwa au kuyarusha. kwenye mtandao Unaweza kufanya hivi kwa kuchora msitari kati kati ya karatasi. kisha ukawa na maombi upande mmoja na majibu upande mwingine Inafurahisha na. kujenga imani unapoona jinsi Mungu anavyojibu maombi yaliyoorodheshwa. Himiza na kukuza hali ya kucho kwa wanakikundi Tunakabili chumba chenye kiti cha. enzi cha Mfalme wa ulimwengu Hebu tusichukulie kipindi hiki cha maombi kwa. uzembe katika mkao wetu au mwenendo Sio lazima kwamba kila mtu apige magoti. muda wote watu na wauone muda huo wa maombi kama muda maalum wa. kufurahisha hivyo wahimize watu wapige magoti au kukaa au kusimama kadiri. Mungu atakavyowaongoza na kulingana na anavyoona nafuu kwake. Maombi kwa Sentenso, Maombi na yawe mafupi na yaelekezwe moja kwa moja kwenye hitaji Kufanya hivi. kutawapatia wengine pia fursa ya kuomba Jaribu kufupisha ombi lako kwa sentenso. chache kila mmoja anaweza kuomba mara kadhaa Maombi mafupi yatafanya kipindi. cha maombi kuwa cha kufurahisha na sio cha kuchosha huku mkimruhusu Roho. Mtakatifu kugusa vikundi na kuwaongoza akiwaonesha namna ya kuomba Sio lazima. kuanza na kumaliza kwa maneno Mungu wetu mpendwa na Amina kwa sababu ni. maombi endelevu kwa mawasiliano na Mungu, Wewe kama kiongozi sio vema utawale kipindi cha maombi Lengo kubwa ni. kuwawezesha wengine kuomba Kipindi cha ukimya kina thamani kubwa ajabu kwani. kinampa Mungu muda wa kuzungumza na mioyo yetu Ruhusu Roho Mtakatifu. afanye kazi kwa kumpa kila mmoja muda wa kutosha wa kuomba. Nyimbo za hapa na pale kutoka kwa vikundi zikichanganywa kwenye maombi. zinaongezea uzuri wa mkutano wa maombi Nyimbo zinazofaa ziorodheshwe kabla ya. kipindi sio lazima ziimbwe zote ila kwa wakati muafaka kama itakavyohitajika. Kuimba pia ni njia nzuri ya kuhama kutoka kwenye kipindi kimoja kwenda kwenye. kipindi kingine,Kukusanya Mahitaji ya Kuombea, Usiulizie mahitaji ya kuombea kutoka kwenye kikundi Badala yake waambie watu.
wataje mahitaji yao katika maombi na kuwahimiza wengine kujiunga wakikubaliana. nayo kwa kuungana katika maombi kimya kimya Sababu kubwa ni kwamba muda. unaweza usitoshe kwa kuombea mahitaji ya mtu mmoja mmoja Ukitaka kuzungumza. kuhusu mahitaji ya kila mmoja unaweza kutumia muda wote wa maombi Shetani. anafurahi anapoona tunatumia muda wa maombi kuzungumza kuhusu matatizo yetu. badala ya kuombea hayo matatizo Wanakikundi wanaweza kuanza kushauriana na. kupendekeza ufumbuzi Uwezo unatoka kwa Mungu Kadiri tunavyoongeza maombi. ndivyo anavyoachia uwezo wake,Muda wako wa kila siku. Ni muhimu wewe kama kiongozi kuhakikisha unatumia muda wako mwingi katika. miguu ya Yesu ukizungumza naye na kusoma Neno lake Ikiwa utafanya kumfahamu. Mungu kuwa kipaumbele chako katika maisha utafunguliwa uzoefu ulio mzuri wa. ajabu Nguvu ya ajabu inayoweza kutingisha dunia hutoka katika sehemu yako ya siri. ya maombi na kuleta matengenezo makuu Pale mahali pa siri akiwa katika utulivu. mtumishi wa Bwana anaweka miguu yake katika mwamba wa ahadi za Mungu The. Great Controversy uk 210,UTANGULIZI, Karibu katika siku kumi za maombi mwaka 2018 Tunamshukuru Mungu kwamba. tunaweza tena kuuanza mwaka huu kwa maombi Mungu amefanya miujiza miaka. iliyopita kwa kadiri tulivyomwomba kwa kufunga Roho Mtakatifu ameleta uamsho. uongofu na shauku mpya ya uinjilisti na uponyaji katika mahusiano yetu Kusema. kweli katika maombi ndipo mahali ambapo uamsho huzaliwa. Tunaamini kwamba maisha yako na maisha ya wale unaowaombea yatabadilishwa. kadiri unavyojiunga na washiriki wengine wa kanisani kwako katika kuomba. kumwagwa kwa Roho Mtakatifu ambaye Baba yetu ameahidi kuwapa wale. Mada yetu ya Maombi Kuhani Wetu Mkuu, Katika siku hizi kumi za maombi tutapitia na kuona kwamba mavazi ya Kuhani Mkuu. wa Agano la Kale yanatupa fundisho gani, Tunasoma katika Tumaini la Vizazi vyote kwamba Kila vazi alilovaa kuhani lilitakiwa. kuwa kamili bila waa lolote Kwa mavazi mazuri hayo yaliyokuwa rasmi tabia ya Yesu. Kristo iliwakilishwa Kile kilichoonekana ni ukamilifu wa mavazi na mwonekano kwa. maneno na kwa roho ili aweze kukubalika mbele za Mungu Yeye ni Mtakatifu na. utukufu wake na ukamilifu wake ni lazima uwakilishwe katika huduma ya hapa. duniani Ni ukamilifu pekee ndio ungewakilisha ule utakatifu wa huduma ya. mbinguni Desire of Ages uk 705, Kila vazi alilovaa kuhani na kila huduma aliyofanya ilikusudiwa kuacha mguso wa.
namna fulani kwa watu Kila kitu kilichohusishwa na vazi na mwenendo wa kuhani. kilikusudiwa kuacha mguso kwa watazamaji wapate kutambua utakatifu wa Mungu. udhati unaohitajika katika kumwabudu na usafi unaohitaj. Sherehe za Sabato ya kuhitimisha Sabato ya mwisho ipangwe mapema uwe ni wakati wa kujumuika katika furaha ya mambo yote aliyoyatenda Mungu katika kipindi hiki cha maombi ya siku kumi Tenga muda wa kutosha kwa ajili ya ushuhuda wa maombi yaliyojibiwa kwa ajili ya mafundisho maalum ya Biblia mahubiri yaliyotayarishwa vizuri kuhusu umuhimu wa maombi na nyimbo za sifa kwa Mungu wetu

Related Books