KAMUSI

Kamusi-Free PDF

  • Date:21 Feb 2020
  • Views:516
  • Downloads:0
  • Pages:251
  • Size:3.00 MB

Share Pdf : Kamusi

Download and Preview : Kamusi


Report CopyRight/DMCA Form For : Kamusi


Transcription:

Hakimiliki IDPC 2016, Haki zote zinamilikiwa na Inclusive Development Promoters. Consultants IDPC,S L P 10211 Dar es Salaam Tanzania. Barua pepe idpc94219 gmail com,ISBN 978 9987 9974 1 1. Toleo la Kwanza 2016,Chapisho hili haliuzwi, Kamusi hii imeandaliwa mahususi kwa watu wote wenye ulemavu. Usanifu na Uchapaji,Nesmap Printing Technology,S L P 70783 Dar es Salaam T.
Baruapepe nesmaptz gmail com, apo inakadiriwa kuwa takribani watu bilioni moja1 duniani ni wenye. ulemavu idadi ya watu wenye ulemavu nchini haikuweza kuwa bayana. kwa kipindi kirefu kutokana na sababu mbalimbali zikichangiwa na elimu. ndogo kwa wahojiwa ambao walitakiwa waeleze ukweli wa hali ya ulemavu kwa. wanafamilia wanakaya Kadiri siku zilivyokwenda hali hii ilibadilika ambapo. Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 na hasa utekelezaji wa Mkakati wa. Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania MKUKUTA ndio matukio. ya awali yaliyochachawiza zaidi matakwa ya kitakwimu nchini kuhusu kundi hili. Kwa umuhimu wake na kwa kuzingatia sera za Taifa za Watu wenye Ulemavu. ya Mwaka 2004 Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilibeba dhamana kwa kuendesha. utafiti mahususi wa Watu wenye Ulemavu mwaka 2008 na kubaini kuwa kundi. la watu wenye ulemavu ni asilimia 7 8 ya idadi ya Watanzania wote Aidha. matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 yamebainisha kuwa. kundi hili ni asilimia 9 3 ya Watanzania wote nchini Ni wazi kuwa ulemavu. uliotambuliwa zaidi kwenye utafiti wa mwaka 2008 na 2012 ni ule wa. kuonekana Imedhihirika kuwa bado kuna idadi kubwa ya Watanzania wenye. ulemavu wa kutoonekana bayana mathalani matatizo ya afya akili uzee. magonjwa ya kudumu kama vile kifafa magonjwa ya kusendeka n k ambao. bado hawajatambuliwa wakati hali zao zinaangukia kwenye kundi hili Takwimu. hizi zimethibitisha pasi na shaka kuwepo kwa kundi hili kama sehemu stahilifu. na ya kudumu katika jamii ya Kitanzania Kwa uelewa huu jitihada za. ujumuishaji wa kundi lenyewe zimeshika kasi kuliko muda mwingine wowote. Pamoja na umuhimu wa takwimu za Watu wenye Ulemavu ni vema kila ngazi. ya utungaji sera na utoaji uamuzi ikazingatia nasaha ya kwamba idadi kamwe. haiwezi kuathiri madai ya haki ya ujumuishaji Kundi hili liwe ni asilimia mbili au. kumi na hata zaidi bado ukweli ni kuwa linakabiliwa na matatizo ya kipekee. tofauti na raia wengine na daima matatizo haya ni matokeo ya kutengwa na. mtazamo hasi wa jamii dhidi yake Suala la msingi hapa ni lile la haki za. binadamu ambalo tafsiri yake ni ya kiulimwengu Katu malengo mbalimbali ya. Kitaifa na Kimataifa hayawezi kufikiwa iwapo hapatakuwapo na mipango. madhubuti ya ujumuishaji wa kundi hili kwenye michakato ya kimaendeleo 2. 1 World Report on Disability 2011, 2 EC Study of Disability in EC Development Cooperation 2010 pg 27. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepokea fursa hii nyingine iliyotunukiwa na kuwa. sehemu ya kujielimisha zaidi kuhusu jamii nzima ya watu wenye ulemavu. Fursa hii imetolewa na Waandishi wa Kamusi Elekezi ya Ulemavu kwa kuiomba. Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwaandikia dibaji ya toleo la Kwanza la Chapisho. hili Kuijumuisha Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuandika Dibaji ni kutoa. uelewa na kupanua wigo mpana kwa Watakwimu ambao utasaidia wakati wa. kuandaa utafiti kuhusu watu wenye ulemavu namna ya kufanya uchambuzi na. kusambaza takwimu zenyewe katika kupanga mipango ya maendeleo kwa. jamii Kwanza Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaunga mkono jitihada zilizofanywa. na Asasi ya Uenezi na Ushauri kuhusu Maendeleo Jumuishi Inclusive. Development Promoters Consultants Juhudi hizi zinaipatia jamii na hasa. watunga sera wapanga mipango ya maendeleo na watoa uamuzi marejeo. mahususi kuhusu kundi hili yenye fasiri inayobeba mtazamo wa wahusika. wenyewe Pili matokeo ya jitihada hizi ni ushahidi kwamba kundi hili linao. uwezo wa kufikiri kubuni na kutenda sawa na Watanzania wengine bila kujali. maumbile hadhi ya kiuchumi na kijamii, Sambamba na hilo chapisho hili litakuwa msaada mkubwa kwetu tulio na. wajibu wa kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu. 2006 ulioridhiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sanjari na utekelezaji. wa Agenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu itakayoishia mwaka 2030. Dhana kuu zote zimetafsiriwa na Kamusi hii kwa mapana Aidha. mnyumbulisho wa aina za ulemavu na mahitaji yake umetolewa kwa kina. Zana imepatikana hivyo ni vyema ikatumika kikamilifu ili kuwezesha matumizi. halisi ya lugha inayotakiwa kwa kundi hili la walio na ulemavu nchini na duniani. kote Ni matumaini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwa Kamusi hii itaendelea. kuboreshwa zaidi hivyo maoni na ushauri uwasilishwe IDPC. Mkurugenzi Mkuu,Ofisi ya Taifa ya Takwimu, amusi hii ni zao la tafakuri na jitihada kubwa za asasi ya IDPC katika. kujaribu kutafsiri kwa vitendo matazamio na dhima yake kuhusu dhana. ya maendeleo jumuishi hususani kwa watu wenye ulemavu Kama. usemavyo msemo wa Kiswahili Mpango si matumizi Msemo huu. unahadharisha kwamba kuwa na wazo fulani pekee hakuwezi kutoa matokeo. yanayotumainiwa endapo hazitakuwepo jitihada za wazo lenyewe kufanyiwa. kazi kivitendo Pia ili kutenda sharti pawepo na rasilimali zinazohitajiwa na. mwenye wazo ama kwa kuzimiliki au kuchangiwa na wengine Halikadhalika ili. kuweza kuchangiwa msingi wake ni mhusika kuwa na uhusiano mzuri kwenye. jamii na jumuiya inayomzunguka, Katika hatua za awali IDPC ilikuwa na wazo la nini kifanyike bila kumiliki.
nyenzo au rasilimali za kutekelezea wazo lenyewe isipokuwa uhusiano mwema. na watu Kutokana na msingi wa uhusiano huu mzuri nakisi ya rasilimali. ilichangwa na wazo likatafsiriwa kivitendo na matokeo yake ni kuchapishwa. kwa Kamusi Elekezi ya Ulemavu Kutokana na ukweli huu IDPC inawiwa sana. na mtu mmojammoja makundi na taasisi mbalimbali Japo kiutaratibu. itaonekana kuwa asasi hii IDPC ndiye mmiliki wa Kamusi lakini kiuhalisia ni. kwamba tunda hili linamilikiwa na wengi ambao bila mchango wao wa hali na. mali tunda lenyewe lisingepatikana, Kutokana na wingi wa wachangiaji haitakuwa rahisi kuwaorodhesha wote kwa. majina Hapa tunatoa shukurani za dhati na za jumla kwa kila mmoja. aliyechangia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hii. Wachangiaji wote katika ujumla wao tunawashukuru sana kwa uzito sawa Hata. hivyo wapo wachangiaji wachache binafsi na taasisi ambazo lazima zitajwe. kwa majina Tuanze kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko wa Maendeleo. wa Watu wenye Ulemavu wa nchini Ufini Abilis Development Aid for People. with Disabilities Bila mchango wa Asasi hii wa kifedha ushirikihali na. ushajiishaji mradi huu ungeishia kwenye hatua ya dhana tu Pia hatuna budi. kuwataja Bwana Batista Mgumba na Godfrey Emmanuel kwa kuudhamini mradi. huu kwa mujibu wa masharti ya Mfuko wa Maendeleo wa Watu Wenye. Ulemavu wa Ufini Wadhamini hawa walifanya hivyo kwa imani tu kwani wazo. lenyewe lilikuwa bado kwenye maandishi tu Mbali na udhamini watu hawa. walijitolea kuufuatilia utekelezaji wa mradi huu kwa hatua zote ili kuhakikisha. kuwa utekelezaji wake unafanyika kwa kadiri ya makubaliano Mabibi Frida. Silumbe na Nuru Awadhi walijipambanua kuwa wajumbe wa kamati ya mradi. iliyohusika na usimamiaji wa mradi wenyewe siku hadi siku Wazee waliobobea. katika nyuga za lugha adhimu ya Kiswahili na uandishi yaani Amir Sudi. Andanenga na John Mbonde ndio hasa waliojenga msingi wa kazi nzima kwa. kubaini visawe na vitomeo vya lugha lengwa vyenye kushabihiana na vidahizo. vya lugha chanzi Kadhalika kila ilipolazimu walibuni istilahi mwafaka na. kuhariri kazi ya uandishi kwa kila hatua, Mabingwa wa lugha ya Kiswahili Mwalimu Elizabeth Mahenge na Bwana. Mayolwa John Nzala walikubali kushirikiana na IDPC kwenye mradi tangu. hatua za awali na kuendelea nao muda wote wakishauri jinsi ya kuufanikisha. Pia tunawashukuru wajumbe wa Kamati ya Ushauri na kikosi cha wataalamu. ambao taaluma zao zinawahusianisha sana na masuala ya ulemavu matabibu. walimu wataalamu wanasayansi ya jamii wanaharakati n k waliojitolea muda. wao kuupitia muswada kwenye hatua zake za awali na kuuboresha kwa kiasi. Shukurani pia zinaelekezwa kwa Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi. zilizokubali machapisho yao kutumika katika kurutubisha uandishi wa Kamusi. hii kwa kuyanukuu au na kuyanakili kila ilipotakiwa Taasisi hizi ni pamoja na. Jumuiya ya Ulaya Ecumenical Disability Advocates Network Wachapishaji. wa vitabu vya Hesperian Sekretariati ya Mkataba wa Haki za Watu wenye. Ulemavu Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa Chama. cha Watu wenye Ulemavu Singapo Disabled People Association Singapore. Ofisi ya Tanzania ya Huduma za Msaada wa Kimataifa International Aid. Services IAS Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Chuo Kikuu cha Dar. e s Salaam na Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA Ni wazi kuwa bila. kukubaliwa kutumia stadi za taasisi hizi uandaaji wa Kamusi hii. usingewezekana kukamilika katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja na wala. chapisho hili lisingekuwa na ubora lilionao Pia BAKITA limeenda mbele zaidi. kwa kuhariri muswada na kuipatia ithibati Kamusi hii. Pia kwa dhati kabisa tunakiri kuwa baadhi ya vielelezo vya kukolezea ufahamu. katika Kamusi hii vimenakiliwa kutoka Mfuko wa Abilis nchini Ufini. Wachapishaji wa Hesperian wa nchini Marekani na kwenye agobui kikoa. public domain web sites Kwa hiyo tunachukua fursa hii kutambua na. kuheshimu hisani ya wote waliosawiri vielelezo hivi na kuvipakia kwenye agobui. tajwa Hapa tunaorodhesha vielelezo hivyo kimojakimoja kutoka agobui kikoa. ambavyo ni abakusi njia fikivu msalani fikivu stadi za kila siku kicharazio. mbadala liftitanga tanzi la mkono athetosisi ubambahimo kizuzizi bakora. ubongo mkuu wayopindu kombeo amirishi pagaro wenzokongojea kionyi. bainifu ubongo mkuu matende vifunza mitembeo mbwa mwongozaji. kingogemeo aina za shimesikio hidrosifelasi ngirimaji hiparopia mkingamo. ufikivu isojinsi kiegemeo dekezi pagaro kiuno mikrosefali ufikivu wa. maegesho tezi dume roleta mfumo wa upumuaji kitobozi supinesheni. mchoro mpapaso vibamba mpapaso kitumi cha mawasiliano kwa viziwi. mpapaso ufahamu trakeostomi kitufe onyeshi video kalimani lugha ishara. kiunzi egemeo kitimwendo vinyanyua vitimwendo ngazimbetuko ya. kitimwendo Anwani kamili za tovuti zilizotumika zimeorodheshwa mwishoni. mwa chapisho hili, Tunapenda pia kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa IDPC ndugu. Rutachwamagyo Kaganzi ambaye alibeba mradi huu mabegani kwake tangu. likiwa wazo hadi kufikia hatua ya mwisho ya kuwa na Kamusi Elekezi ya. Ulemavu mikononi Mchango wake haumithiliki katika kazi hii kwani ilifanyika. katika mazingira magumu ya kutokuwapo kwa rasilimali stahilifu za kutosha Ni. moyo wa kujitolea na ubunifu wake ndivyo vilivyouvusha mradi huu kwenye. milima na mabonde, Mchapishaji wa kazi hii naye anapewa shukurani za pekee kwa ushirikihali. wake na jitihada za kuhakikisha kuwa kazi inakamilika katika muda uliopangwa. Rutachwamagyo Kaganzi,Mkurugenzi Mtendaji,Januari 2016.
Mwongozo wa Kutumia Kamusi Elekezi ya Ulemavu, amusi hii ni elezi kwa mantiki kwamba inaelezea hisia za watu wenye. ulemavu Imetoa taarifa juu ya ulemavu wa aina mbalimbali ili jamii iweze. kujitanabaisha na masuala anuwai yanayohusu ulemavu na athari zake. Mwansoko na wenzake 2013 uk 11, Hii ni Kamusi amili kwani inachochea hisia za wanajamii kuwa chanya kuhusu. ulemavu Aidha ina vionjo vya kiinsaiklopia kwa vile maelezo na ufafanuzi. wake huzama ndani zaidi kuhusu dhana kadha wa kadha zilizomo humu kwa. lengo la kutoa maarifa ya kisayansi kiuchumi kitaaluma n k na hivyo kuifanya. kuwa chombo pekee na marejeo muhimu katika uga huu wa ulemavu ibid. Kamusi Elekezi ya Ulemavu ina lugha mbili Kiingereza lugha chanzi na. Kiswahili lugha lengwa, Kwa kiwango kikubwa Kamusi hii inazingatia matumizi ya adabu lugha na. akhlaki za ulemavu kutokana na ukweli kuwa suala zima la ubaguzi kwa. misingi ya ulemavu limejikita kwenye hisia kuhusu hali hiyo na wahusika wake. Mtu au jumuia hudhihirisha hisia walizonazo kuhusu ulemavu kwa njia ya lugha. inayoamuliwa kutumika kuielezea hali au mhusika mwenye kilema Kwa mantiki. hiyo lugha inayotumiwa huwa ndio msingi wa kujenga mila na utamaduni. mahalia Ndiyo maana katika Kamusi hii istilahi msamiati au maelezo yenye. kukirihisha kwa mtu mwenye ulemavu yamewekewa alama ya vinyota viwili. mbele yake kama utambulisho maalumu kuwa hayapaswi kutumika kwa. mfano mguurungu Kwa kulizingatia hili Kamusi hii imeandaliwa kwa jicho la. ulemavu na hivyo kukidhi matakwa ya walengwa kuhusu kasoro za adabu. lugha maana ashirifu na mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu. Aidha ndani ya Kamusi hii kuna vidahizo na visawe vilivyoibuliwa na kubuniwa. na taasisi za taaluma maalumu k v BAKITA TATAKI n k ambavyo viliingizwa. kwa makubaliano yaliyofanyika baina ya IDPC na mamlaka hizo ili kukidhi. taratibu na kanuni za haki miliki Nukuu za aina hiyo zimewekewa tarakimu za. Kirumi mwishoni mwa kila nukuu na kuandikwa jina la mamlaka inayohusika. kurasa za mwisho wa Kamusi hii mathalani BAKITA Kamusi Kuu ya. Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa Dar es Salaamu 2013 uk 8. Uundaji wa Kamusi hii ulihusisha, i Uainishaji wa vidahizo dhana semi istilahi kutoka lugha chanzi. Kiingereza, ii Utafutaji na uainishaji wa visawe na vitomeo vya lugha lengwa.
iii Uundaji wa istilahi mpya za Kiswahili ilipobidi kufanya hivyo au. kutumia msamiati wa lugha za Kibantu unaofanana na dhana. inayofafanuliwa mathalani visawe vya nsiso kimina na ntenga. kingogemeo aina za shimesikio hidrosifelasi ngirimaji hiparopia mkingamo Hii ni Kamusi amili kwani inachochea hisia za wanajamii kuwa chanya kuhusu

Related Books